ENCC SABAOTH
Ni idara ya vijana inayolenga kuwaunganisha vijana wote wa ENCC katika kumtumikia Mungu kwenye huduma mbalimbali kanisani, 1 Yohana 2:14. Idara hii ni ya baraka makanisani kwani kupitia idara hii vijana wanapata kujifunza wajibu wao ndani ya Kanisa na kuwa na moyo wa kumtumikia Mungu.
Sifa za Vijana wa Sabaoth
• Kijana yeyote mwenye umri kati ya miaka 13 na 45
• Awe amezaliwa mara ya pili
• Awe mshirika wa ENCC
Lengo Kuu
Kumjenga kijana wa ENCC katika imani thabiti ya Kikristo ili aishi maisha matakatifu na yenye ushuhuda na mfano wa kuigwa katika jamii. Kumwandaa kijana kuwa mtumishi na kiongozi wa siku zijazo.
Kalenda ya Sabaoth
• Juni: Kongamano la Kitaifa
• Aprili: Kwenda na mawindo kupokea baraka, ngazi ya Kitaifa
• Oktoba: Kwenda na mawindo kupokea baraka, ngazi ya Kanisa