Familia ya Agano Jipya Inayoishi Kimaagano
Kuanzia askofu wetu, viongozi wetu, wachungaji wetu, makanisa yetu, na kila mwanafamilia, Elim New Covenant Church - Tanzania ni kanisa la agano jipya lenye wanafamilia tunaoliishi agano katika kila eneo la maisha yetu kwa neema na rehema za Mungu Baba, na kuwezeshwa kwa Mungu Roho Mtakatifu, katika jina la uweza la Yesu Kristo (Mungu Mwana).
MOYO WA WANAFAMILIA YA MJI WA BWANA
Kuwapenda watu wote kwa upendo usio na masharti wala ubaguzi. Tunayaishi maagano ya Mungu wa maagano kwa namna isiyo ya kupapasa. Tunajidhabihu kwa sadaka zetu, imekuwa ni maombi yetu na shauku yetu kuwafikia walio mbali kwa vipindi vya TV, redio, mitandao ya kijamii na vipeperushi.
MSINGI WA MADHABAHU
Isayah 25:6–7, na katika mlima huu Bwana atawafanyia mataifa karamu ya vinono. Bwana ameiinua Madhabahu ya Mji wa Bwana na kuuita kwa jina lake. Amechagua kulikalisha jina lake, akisikia maombi ya watu wake wanaomuita tokea mahali hapa, 2 Nyakati 7:15–16. Ni Madhabahu yenye kumdhihirisha Mungu wa kweli kwa ibada zenye mdhihirisho wa matendo makuu ya ishara na ajabu kwa kumwabudu katika roho na kweli, kwa kusifu, kuabudu Neno lililo hai, maombi, kuomba na maombezi. Madhabahu ina mlinzi wa Madhabahu ambaye ni Malaika wa Mungu anayebeba maombi yako na kuyafikisha mbele za Mungu, nawe kuyapokea majibu yako.
SHUHUDA
Mungu amewafungua wengi walioonewa na nguvu za giza, magonjwa, mapepo na shetani, nguvu za mauti na chochote chenye misingi ya uovu hung’olewa. Wengi wamepokea watoto na kurejeshewa furaha ndoa zao. Vijana wameoa na kufurahia ndoa zao, mabinti wameolewa na kuwa baraka kwa wenza wao. Zaburi 101:8, asubuhi hata asubuhi nitauangamiza uovu wote wa nchi…utatengwa na kila uharibifu. Isaya 60:14, wale wote waliokutesa…watakuja na kukuinamia. Zaburi 48:8, kama tulivyosikia, ndivyo tulivyoona, Mji wa Bwana utaona kama ulivyosikia, shuhuda zake kuu. Utaitwa MJI WA BWANA, Sayuni Mtakatifu wa ISRAELI.
KALENDA YA MAJUMA YA KINABII (MATUNDA 12 KWA MWAKA)
Kutana na Mungu kwa kila juma la mwisho wa mwezi, kila mwezi kuanzia Januari mpaka Desemba, kwa mwaka mzima. Tukijidhabihu kwa kufunga na kuomba, maombi na maombezi, tukikutana Madhabahuni kila jioni, tukikutana na mguso wa Mkono wa Mungu na kufanywa watu wengine. Hakika maisha yetu hayatabaki kama yalivyo.