Hebron TV

The Mountain of Peace and Excellence

Inapatikana StarTimes Antenna, Channel 416

Calebs Tuongee

Kipindi cha Calebs Tuongee kinazingatia urejeshwaji wa baba kama kichwa na nguzo ya familia. Kuwakumbusha wanaume juu ya huduma yao na nafasi yao katika kujenga ufalme wa Mungu. Kupitia mada na mijadala mbalimbali, chunguza jinsi mwanaume anavyomwakilisha Kristo vizuri katika jamii inayomzunguka na kupata jukwaa la kushiriki yote ambayo anapaswa kufanya kama baba.

Abigaili Anaongea

Nani ni Abigaili wa leo? Anafanya nini na anawezaje kuendelea kushikilia nafasi na hadhi yake katika ulimwengu na mabadiliko ya sasa? Je, Abigaili wa leo anaweza kuwa mwenye busara, mwenye nguvu, mkarimu, na mnyenyekevu kama yule tunayesoma kuhusu katika 1 Samweli 25? Jiunge na Binti Abigaili, huduma itakayokusaidia kuchunguza maana ya kuwa Abigaili wa kisasa kupitia kpindi cha Abigaili Anaongea.

Sabaoth na Hatima Yake

Vijana wenye heshima na utukufu walio jasiri katika Kristo, vijana wa Sabaoth ni jeshi kuu la Mungu. Sabaoth hawauzurii kanisani na kuacha walichojifunza hadi ibada inayofuata bali kwa neema ya Mungu huyaishi wajifunzayo. Jiunge na huduma ya Sabaoth wakichunguza mada na changamoto mbalimbali za ujana na maisha ili kuwasaidia vijana kuimarisha utambulisho wao katika Kristo.

Watch Live Services

Fields marked with an * are required