Lengo Kuu

Kurejeshwa kwa baba kama kichwa cha familia, kama nguzo ya familia, katika dhumuni kuu la baba katika kanisa na utumishi. Kumkumbusha mwana Caleb’s kuwa kazi hii inatuhusu na kutumika katika kuujenga ufalme wa Mungu. Si hivyo tu, bali kumuwakilisha vyema Kristo katika jamii inayomzunguka mbali na kupata jukwaa la kuweza kushiriki yale yote yampasayo kutenda kama baba. Kwa kukumbushwa nafasi yake katika kanisa na katika jamii atakuwa baba bora katika familia hata kuweza kuwafikia wengi ndani na nje ya kanisa.

Sifa za Mwanaume wa TCG

• Awe ameoa na ni mshirika wa kanisa la ENCC
• Awe na mke mmoja
• Awe ameokoka
• Awe mwaminifu

The Caleb's Group (TCG)

Maono
Maono

Maono na utume wa TCG ni kuwa na mwanamume aliyerejea katika nafasi ya awali ya uumbaji wa Mungu (Mwanzo 1:26-28), na ambaye ni sifa na utukufu wa Kristo kupitia maarifa ya kumjua Yeye (2 Wakorintho 2:15).

Urejesho
Urejesho

Kuona kuwa wanaume wanapata uponyaji binafsi kutokana na majeraha (woundedness) na dhambi zisumbuazo maisha yao kupitia semina, warsha, makongamano, machapisho, na faragha (retreats).

Utendaji
Utendaji

Kuwa na mikutano midogo na mikubwa ya wanaume iliyoandaliwa na kuendeshwa kwa ubora mara hapa ENCC–Mji wa Bwana kwa ajili ya maombi, kujifunza Neno la Mungu, kuhubiri injili, kuinuana, na kutiana moyo pamoja na mijadala mbalimbali ya maendeleo ya mwanamume.

Mafanikio na Maazimio TCG

Idara imejenga umoja baina ya wababa kwa kuchangiwa na kukutana mara kwa mara. Hii husaidia kujenga ushirika ambapo kwa kutumia jukwaa hili la kiidara tunaweza kuwafikia wenzetu wanaopata shida za kifamilia kama magonjwa na misiba kwa kushiriki kwetu na kuzitumia rasilimali zetu katika kuzifariji familia hizo.

Wana Caleb’s hawaachi kujihusisha na wenzetu katika maswala yote yenye kusherehekewa, kama harusi, n.k.  Hii inawafanya wana Caleb’s na jamii ya ENCC kujisikia salama kama familia yenye kuuishi upendo wa Kristo katika maisha yetu.

Umisheni ni moja ya malengo ya The Caleb’s Group katika kuujenga ufalme wa Mungu kwa kuwafikia ambao hawajafikiwa kulitimiza agizo kuu la Bwana wetu Yesu Kristo. The Caleb’s imefanikiwa kuwa na wawakilishi katika mkutano uliofanyika kule Muheza ambapo tuliruhusu rasilimali zetu kumtumikia Mungu, na ni mpango wa The Caleb’s kuendelea kufanya hivyo. Kadhalika katika umisheni, The Caleb’s tumeweza kutegemeza kwa sadaka zetu mkutano wa injili Mbagala kwa Mch. Mwaitela.

The Caleb’s hushiriki kikamilifu katika The Marriage Summits, na hakika tunaona matunda yake. Wana Caleb’s hivi sasa wana Tabasamu la Kiuungu kuliko ilivyokuwa kabla ya Marriage Summits.

Pia, tunaangalia njia iliyo bora ya kuwafikia walio wengi kwenye Makanisa ya ENCC na Parishi nyingine kwa ujumla. Hii itasaidia mpango wa Kupata na Kubadilishana Mawazo (Exchange Experience Program), maana huko nako tunaamini wako Caleb’s wengi wanaohitaji kumtumikia Mungu endapo wakipata fursa.

Kalenda ya TCG

Septemba: kwenda na mawindo kupokea baraka, ngazi ya Kitaifa