Upanga wa Bwana

Yeremiah 47:6; 1 Wafalme 3:24; 1Nyakati 21:12; Isaya 34:6; Ufunuo 19:15

Matamshi ya Kiunabii na Bishop Dr. Manasse DM

Haya ndiyo yale naliyopokea kutoka kwa BWANA,

2023, Upanga wa BWANA unaondoka alani mwake ili Mungu aamue uzuri wa wale wanao muabudu yeye, na hukumu ya wale wasio mcha yeye. Mwaka huu kando ya yale ambayo Mungu anataka kuyatetea, Upanga wa BWANA unaenda kusimama katika anga la taifa na mataifa kwa ajili ya kutazama maisha ya watu na usafi wa tabia katika maisha ya watu kwa kuwa huu ni mwaka ambao ufalme ule wa giza umewavuvia watu kuachilia aina ya ushawishi wa kipepo wenye lengo la kupotosha mioyo na maisha ya watu.

Ushawishi wa kipepo kwa wale walio katika madaraka na vyeo wapo katika hatari iliyo kubwa. Hii ndiyo sababu iliyopo katika moja ya siku, nimeona farasi mwekundu aliyepandwa na mtu mwenye mavazi meupe, hii ni satanic seduction. Shetani anapojaribu kuwashawishi watu kama ana nia nzuri, kumbe nia yake ni Upanga, nia yake ni mauti – na BWANA kabla hajaruhusu ushawishi huo kuzaa matunda yake, Upanga wa BWANA utakuwa umesimama katika njia ya watu hao wanaoshawishi mabaya.

Mwaka huu ndiyo mwaka ambao, watu watakuwa wamekosa utulivu na kukosa maadili. Maisha ya watu yanaenda kuwa yametatanika, utashangazwa kuona watu walioheshimiwa, watu waliotazamiwa wanene hekima wanaenda kuwa watu wanaonena maneno yasiofaa na ya kupuuzwa na wote, kwa sababu Upanga wa BWANA unaenda kufichua yaliyopo mioyoni mwao, na siyo yale yanayoonekana kwa macho ya damu.

Mwaka huu ndiyo mwaka ambao, Mungu anapouachilia upanga anakusudia kukutana na ghadhabu na nia ya tumbusi (satanic vulture) kwa sababu kumekua na mauaji ambayo hayana maana yoyote. Mwaka huu aina ya wanadamu wanaoondoa uhai wa wengine bila ya sababu wanaenda kuinuka. Na hivi ndivyo huvutia Upanga wa BWANA kutetea damu inayomwagika juu ya uso wa nchi kinyume cha hao wanywao damu na wanaosikia raha kupoteza uhai wa wengine.

Mwaka huu ndiyo mwaka ambao hali ya watu kuchanganyikiwa na kuenenda kwa kukosa mwelekeo itazidishwa sana kwa sababu ya watu waliojitoa katika mkono wa muovu ili wamtumikie kwa nguvu zao zote. Upanga wa BWANA unaposimama kuwaandama, ili kuongeza zaidi wazimu wao, ni kwa lengo la kuwafanya wale wanaomcha Mungu wawe dhahiri, na wale ambao ni waongo wanaonena mambo ya nuru lakini wao ni giza wawekwe dhahiri.

Mwaka huu ndiyo mwaka ambao kutakuwako na Upanga wa BWANA kwa wale ambao wameweka ngome zao kwenye madhabahu za kipepo. Hawa ni watu ambao wameweka nadhiri za kumtumikia shetani bila kujali inagharimu nini na kufanya maagano yenye nguvu bila kujali nini. Hii ni kwa sababu shetani ndiye aliyewapa uwezo wa kumiliki vitu na kuwapa uwezo wa kukaa katika madaraka. Upanga wa BWANA hautatulia tangu Januari hii mpaka Desemba, utawaandama na BWANA atamwangusha farasi na mpanda farasi – zitaanguka madhabahu na makuhani wake.

KWA MTU MMOJA MMOJA

Tazamia hila za adui kuinuka dhidi ya wenye haki kwa nguvu zaidi. Hii ndiyo sababu BWANA anauinuia Upanga, ili kusudi yeye aliye na hila afichuliwe, na yeye aliye mwenye haki awekwe dhahiri. Mwaka huu ndiyo mwaka ambao BWANA atawalipizia kisasi watu wake, yale yote uliyopoteza 2021, 2022, na yale yote uliyopoteza nyakati zozote. Kama ambavyo BWANA aliinuka kwa kisasi kwa ajili ya Daniel na wale waliomuinulia hila waliingia kwenye tundu la simba, BWANA ananena huu ni mwaka ambao waovu wote watakutana na kisasi cha BWANA kwa ajili ya walio wake.

Mwaka huu ndiyo mwaka ambao unakupasa kufanya uamuzi ulio wazi kana kwamba utajikuta upo matatizoni basi kile kilichokupa tatizo iwe ni kwa sababu ni mwenye haki na ni kwa sababu ya thamani ya yaliyo ya Mungu uliyoyabeba na sio kwa sababu ya dhambi na hatia zako. Kama utaenda gerezani kama Yusufu mwaka huu, furahi na kumtukuza Mungu kwa sababu agenda ya Mungu inaenda kutimizwa. Kama utajikuta upo kwenye tatizo lolote kwa sababu unachokitetea ni agenda yako na MUNGU, na wenye hila wakakuinukia kwa nguvu zote, furahi kwa sababu mwisho wa yote Upanga wa BWANA utainuka nao utakutetea.

“Chagua kupambana, kataa kujichanganya. Chagua kupambana, kataa kujichanganya.”

Mwaka huu ndiyo mwaka ambao unakupasa kubeba yote ya dhamana za unyoofu wa moyo katika yeye. Fanya uamuzi wakukataa michanganyo, chagua kupambana kuliko michanganyo. Ukijichanganya na wanadamu, mapambano na maovu yatakoma lakini Upanga wa BWANA utakumaliza na hao waovu wanapopotea. Ukipambana nao wanaopambana na agenda ya Mungu, Upanga wa BWANA utasimama upande wako, utawashinda wanaosimama kinyume na agenda ya MUNGU katika maisha yako.

Mwaka huu ndiyo mwaka ambao adui ataleta hali ya mambo na kukuletea watu watakaokuhoji, “Je, Mungu wako unayemtumainia daima anao uwezo wa kukuponya na kukukomboa na haya pia?” Jawabu lako daima lakupasa liwe, “NAAM, BWANA Mungu wangu hakika yake anao uwezo wa kunikomboa na hali hii, nae atanikomboa.”

KATIKA NGAZI YA FAMILIA

Nimeiona timazi ikiwa imewekwa, nimeona mwanzi wa kupimia. Hii ni timazi nayo imewekwa ipime kwa haki na ihimize kikombe cha haki. Wale wote ambao wamekataa uwongo na ulaghai, Mungu atathibitisha kweli yake katika maisha yao. Na wale wote ambao wameweka tumaini lao katika maneno ya uwongo, MUNGU atadhihirisha ya kwamba uwongo kamwe si kitu cha kutumainiwa.
Mungu anataka kudhihirisha, katika ngazi ya kila familia, wale waliopo na wasiokuwepo kanisani. Kila familia iliyoweka tegemeo la ustawi na mafanikio yake katika madhabahu za uovu, ustawi na mafanikio hayo hayatasimama maana katika mwaka huu farasi na mpanda farasi wataanguka na yule anaetegemea msaada wa farasi au mpanda farasi ataanguka pamoja nae pia.

Mwaka huu, inapaswa mzazi kuwa makini na yale unayoyabeba, yale unayoyatenda, na yale unayoyazalisha maana yanaenda kuwa na matokeo kwa watoto wako. Hawakuwa mawaziri tu walioleta hila dhidi ya Daniel waliotupwa katika tundu la simba, walikuwa mpaka wake zao na watoto wao waliotupwa kwenye tundu la simba. Mwaka huu wa Upanga wa BWANA, kosa la mzazi litafanya mpaka watoto waathirike, tazama mwenendo wako mbele za MUNGU, enenda ilivyo vyema ili Mungu anapokutetea atetee na uzao wako pia.

“Mwaka huu, inapaswa mzazi kuwa makini na yale unayoyabeba, yale unayoyatenda, na yale unayoyazalisha maana yanaenda kuwa na matokeo kwa watoto wako.”

Mwaka huu, zile ngome zinazoangamiza familia zinaenda kuinuka kwa kiwango cha juu kabisa, ngome zile zinazopotosha jinsia za watu. Huyu amezaliwa wa kiume, nazo zinasema, “Kuanzia leo umekuwa mwanamke.” Huyu amezaliwa wa kike, nazo zinasema, “Kuanzia leo umekuwa wa kiume. Unaweza kuoa.” Ngome hizi zinaenda kuwa dhahiri katika namna ambayo haijawahi kutokea hata katika bara hili la Afrika na mataifa yake, ndio maana Upanga wa BWANA unainuka. Hii ni kwa sababu yule malkia wa anga ameinuka, nae amemaanisha anataka kuwatumikisha wanadamu kwa jinsia zisizokua zao. Wale ambao wanasikia raha kuondoa uhai wa watoto kwa kutoa mimba na wale wanaosikia raha kuua akili njema za watu kwa kuwavika na kongwa la madawa ya kulevya, hizi ni ngome zinazoua familia zinaenda kuinuka. Hii ndio sababu BWANA ananena mwaka huu ni mwaka wa Upanga wa BWANA, kuna wale ambao hawataweza kupiga magoti kwa maneno tu mpaka BWANA atakapoinua upanga wake kinyume chao. Huu ni mwaka wa Upanga wa BWANA.

Familia ile itakayomruhusu Mungu kutawala, kuweka Madhabahu kuwa maficho yao, na kupaza sauti yao katika maombi ikimngoja Mungu, familia hii Mungu ataipa sauti itakayogusa vizazi, na sauti yao hakuna atakayeinyamazisha. Familia hii inaenda kupewa usemi vinywani mwao kama familia ya Mordecai, Daniel, na Yusufu – watua ambao hila zote zikishakuinuka, Upanga wa BWANA ukiisha kuwatetea, hata katika kunyamaza kwao, sauti ya yale waliyoyaishi itapiga kelele katika taifa na mataifa.

KWAKO ENCC

Mwaka huu, zile ngome zinazoangamiza familia zinaenda kuinuka kwa kiwango cha juu kabisa, ngome zile zinazopotosha jinsia za watu. Huyu amezaliwa wa kiume, nazo zinasema, “Kuanzia leo umekuwa mwanamke.” Huyu amezaliwa wa kike, nazo zinasema, “Kuanzia leo umekuwa wa kiume. Unaweza kuoa.” Ngome hizi zinaenda kuwa dhahiri katika namna ambayo haijawahi kutokea hata katika bara hili la Afrika na mataifa yake, ndio maana Upanga wa BWANA unainuka. Hii ni kwa sababu yule malkia wa anga ameinuka, nae amemaanisha anataka kuwatumikisha wanadamu kwa jinsia zisizokua zao. Wale ambao wanasikia raha kuondoa uhai wa watoto kwa kutoa mimba na wale wanaosikia raha kuua akili njema za watu kwa kuwavika na kongwa la madawa ya kulevya, hizi ni ngome zinazoua familia zinaenda kuinuka. Hii ndio sababu BWANA ananena mwaka huu ni mwaka wa Upanga wa BWANA, kuna wale ambao hawataweza kupiga magoti kwa maneno tu mpaka BWANA atakapoinua upanga wake kinyume chao. Huu ni mwaka wa Upanga wa BWANA.

Familia ile itakayomruhusu Mungu kutawala, kuweka Madhabahu kuwa maficho yao, na kupaza sauti yao katika maombi ikimngoja Mungu, familia hii Mungu ataipa sauti itakayogusa vizazi, na sauti yao hakuna atakayeinyamazisha. Familia hii inaenda kupewa usemi vinywani mwao kama familia ya Mordecai, Daniel, na Yusufu – watua ambao hila zote zikishakuinuka, Upanga wa BWANA ukiisha kuwatetea, hata katika kunyamaza kwao, sauti ya yale waliyoyaishi itapiga kelele katika taifa na mataifa.

“Mpe Yeye utukufu, mpe Yeye utukufu, mpe Yeye utukufu. Hivi ndivyo unavyokuwa silaha za vita vyake mkononi mwake.”

Nalimuona mlinzi ambae ni Simba wa kabila la Yuda. Nami nikaona upanga, nae akanena, “Nimeweka timazi katika kuta zako. Wala unafiki hautakaa ndani yako tena.” Wala watu wale ambao wanamtumikia MUNGU kwa midomo yao lakini mioyo yao iko mbali nae, BWANA anakuita katika magoti ya toba na rehema ya kweli. Nenda mbele zake ukiwa umemaanisha utamuishia yeye katika kweli na si katika namna ya maneno matupu wakati moyo wako uko mbali nae. Ndivyo nilivyoona namna ambavyo Mungu anawaamini wengi kwa hazina za fedha na mali ambazo hawakustahili, hazina za mbingu zimefunguliwa kwa ajili yao.
Wakati upanga ukiwaandama walio gizani, wale wasiofaa, wanaostahili hukumu, BWANA anakuamini kwa fedha na mali. Nae anasema agenda ya kukuamini kwa fedha na mali hizo ni kwa ajili ya kuuthibitisha ufalme wake. Ndivyo ninavyoona Mungu atawatumia wengi kutoka katika familia hii ya ENCC kuyaondoa mabaya yaliyokuwa yawapate wengi.

Nami nikaona wako wale wanaochukiwa mpaka wamejawa na hofu ndani yao kwa kuwa kila mahala wanayoyanena, wanayanena yasiyofaa nayo yanasikika kutokea mbali na habari inawafikia. BWANA ananena dumu katika kujinyenyekeza chini yake kwa kuwa yeye anaachilia wingu la ulinzi wake juu yako na chuki zao hazitakutenda wewe madhara yoyote, agenda yoyote ya kuzimu haitafanikiwa katika maisha yako na shuhuda za yale anayokutendea. BWANA ananena kuwa, hata adui zako watafanywa kuwa rafiki zako.

KWA MWILI WA KRISTO MAHALA POTE PALIPO NA NCHI

Hii ni sehemu ya mambo ambayo imegharimu siku nyingi zaidi. Kwa kuwa mwili wa Kristo umeacha yale Mungu aliyowaitia, mwili wa Kristo ukageukiana wenyewe kwa wenyewe na watu wakatafutana ili kumsaidia shetani kazi ya kuwapiga wale walioitwa na Mungu. Kila mmoja kajifanya kuwa hakimu wa mwingine na kuwa mhukumu wa mwingine. Na BWANA anasema, “U nani wewe umhukumuye mtumwa wa mwingine? Kwa kuwa yeye kwa BWANA wake anasimama.” Na hiki ndicho kilio cha machozi ya moyo wangu mbele za Mungu.

Kanisa, hiki ndicho kizazi kitakachokutana na BWANA Yesu, hiki ndicho kizazi ambacho hakiwezi kustahimili unajisi wowote, hakiwezi kustahimili kubeba mawaa ndani yake, hakiwezi kustahimili kuenenda na michanganyo kwa kuwa ni kanisa safi lisilo na madoadoa ndilo atakalokutana nalo BWANA Yesu.

“Katika midomo ya makuhani uhifadhiwa maarifa, uhifadhiwa hekima, uhifadhiwa suluhisho la maisha ya watu.”

Kwanini kuuza haki ya mzaliwa wako wa kwanza kwa sababu ya vitu vya dunia hii? Kanisa, usiuze haki ya mzaliwa wako wa kwanza. Wewe ni mboni ya jicho la Mungu, rejea na urejeshe ule utukufu wa Mungu uliopotea. Nyakati zimewadia ambazo watu wanapaswa kuuliza tupate wapi usalama? Ndivyo ilivyonenwa katika zamani zile za kale kwamba, “Katika midomo ya makuhani uhifadhiwa maarifa, uhifadhiwa hekima, uhifadhiwa suluhisho la maisha ya watu.”
Kanisa, nyakati za kupuuzwa kwako zimekoma, na nyakati za kusimama kwako zimewadia. Rudi na urejeshe utukufu ule uliopotea. Kanisa haya ndiyo majira ambayo BWANA anasema, “Ondoka kati yao ukatengwe nao, wala usikae katika baraza la wasio haki, wala usiende katika njia za wakosaji, ondoka ukatengwe nao.” Kwa sababu BWANA amekupa onyo kuwa Upanga wa BWANA hautabagua na utaanza kutokea katika nyumba yake mwenyewe. Yeye hatomtazama mtu muovu kuwa kama mtu asiye na hatia na wala yeye hatomtazama mtu mwenye haki kuwa kama mtu mwenye hatia. Rejea, na kicho chako mbele za Mungu kitakuponya na kukuokoa.
Kanisa, Mungu atakuamini kwa hazina za ufalme, zitumie kwa uaminifu, hofu, na kwa hekima. Huku ukijua ya kwamba Mungu ameziachilia hazina hizo mikononi mwako kwa sababu anataka ulete tofauti kwa maisha ya wengi kwa vizazi vingi vijavyo.

KWA TAIFA NA MATAIFA

Nyakati za utungu kwa mataifa ndiyo hizi. Mlisikia imenenwa, nayo imeandikwa, itasikika vita na tetesi za vita. Jambo hili si jambo lililo katika nyakati zijazo tena. Ninyi ni mashahidi kwamba mnaishi katika nyakati hizo, lakini uvuvio huu wa nguvu ya pembe tatu, mwaka huu inaenda kuwapa wazimu zaidi wale ambao wanashikilia madaraka; wala si wao wenyewe kwa sababu nguvu ya pembe tatu inawasukuma kufanya maamuzi yasiyojali thamani za maisha ya watu katika mataifa. Hii ndiyo sababu Mungu anapoinuka na kusema Upanga wa BWANA umeondoka alani mwake, anamaanisha anapambana na miungu walio nyuma ya falme za mataifa.

Wala Mungu hafurahii maangamivu ya mwanadamu awaye yote. Ndivyo katika mataifa kumeachiliwa walao na waharibu kutoka kuzimu. Wana sura za wanadamu, wanafanana na wanadamu, wamezaliwa na tumbo la mwanamke lakini hawa si wenye njaa. Kama wangekua wenye njaa madaraka wakiisha kuyapata yangewatosha, kama wangekuwa wenye njaa pesa walizo nazo zingewatosha, na mtu awaye yeyote akitenda madhara kwa vizazi vya wanadamu kwa sababu ni mwenye njaa rehema ya Mungu itamuangukia. Lakini mtu huyu atendaye madhara kwa maangamivu ya maisha ya wanadamu, iwe ni kwa upanga au kwa njaa akawasababishia magonjwa, akawaletea tauni, huyu si mwenye njaa huyu ni mharibu aliyeitwa kutoka kuzimu. Wameinuliwa kwa maelfu katika mwaka huu kwa lengo la kuangamiza vizazi vya watu, Upanga wa BWANA utasimama kuwazuia.

“Kuna mahala ambapo fedha zitakwisha, kuna wale ambao Mungu ataachilia hazina za utele kwa ajili yao.”

Mwaka huu, wengi wao watatoka waende safari na hawatafika safari hizo, ajali zitayameza maisha yao kwa sababu Upanga wa BWANA umeinuka juu yao. Wengi wao watalala hawatainuka kwa sababu tauni itayameza maisha yao, wengi wao watakaosalia watakuwa na fedheha iliyo wazi, watapelekwa katika mahakama na watawekwa katika magereza wazi – wengine wakiona ili nao wajue kwamba uovu haujawahi kumfanikisha awaye yote.

Mwaka huu ndivyo Upanga wa BWANA utavyokuwa dhahiri ukiwaandama wote wanaomtegemea shetani ili kuwainua na kuwapa chochote cha fahari, iwe ni umaarufu, iwe ni madaraka, iwe ni nguvu. Wenye hila na hila yao, BWANA anaondoa sauti vinywani mwao, hawataweza kuinena hila yao katika saa ya kuinena hila yao. Kanisa zingatia hili, 2025 unaenda kuwa wakati ambao dirisha la neema linaenda kufunguliwa kama dirisha la safina la Nuhu, lakini 2025 haiamui hatima yako. 2024 ni mwaka uliojawa na utimilifu mkubwa wa ahadi za MUNGU na ili ukutane nazo ahadi hizo, misingi yake yote inajengwa sasa.

Mwaka huu ni mwaka ambao Upanga wa BWANA unaposimama unakusudia kumporomosha marmon. Marmon ataanguka na ndivyo utaona uchumi wa mataifa mengi utatikisika kwa namna ambayo haijawahi kutikisika mwaka huu. Kila wakati utakapoona watu wakilia kwa mengi kwamba hali imekuwa ngumu, maisha yamekuwa magumu na kwamba hakuna fedha tena, marmon ataanguka kwa makali ya upanga. Wewe ambae unajua ya kwamba Mungu ndiyo chanzo cha mema yote unayoyategemea, atakuinua tena kama Yusufu.

 

“Mungu hapambani na wanadamu, anapambana na ngome za uovu zilizoinuka ili kuwatumia wanadamu wanaoinuka kuleta madhara kwa vizazi vya wanadamu.”

Huu ndio mwaka unaoenda kuwa na shuhuda zenye nguvu ambazo hujawahi kuziona kwa sababu kuinuka kwa agenda ya kuzimu kwa nguvu kiasi hicho kumeifanya mbingu kuinuka kwa nguvu kiasi hiki. Huu ndio mwaka ambao wale wanaotazamia kupiga mbio kwa umahiri wao, hawataanza hata mbio hizo.

Mwaka huu na uwe mwaka utakaokupa fidia ya chochote kilichoibwa na kupotea miaka miwili iliyopita. Mwaka huu na uwe mwaka utakaoamua matokeo ya shuhuda zako kwa miaka miwili ijayo.

https://www.youtube.com/live/pSmWT9f8NpY?si=4e6BS3KbWepCkEtN&t=2368